Mpanda FM

KATAVI, Bidhaa za Vyakula Vilivyoisha Muda Husababisha Kuhara

24 January 2024, 3:43 pm

Madhara ni  kupelekea  mtumiaji kupata homa na hata kuharisha kutokana na  sumu iliyopo ndani ya Chakula”. Picha Na Mtandao

Na Lilian Vicent-katavi

Baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameeleza maoni yao Mseto juu ya namna wanazingatia muda  sahihi  wa  matumizi ya bidhaa za vyakula kabla Haizijaisha muda wake Wa matumizi.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza Na Mpanda Radio kuwa wanazingatia na wengine wameeleza kwamba  hawazingatii Muda wa matumizi sahihi ya  bidhaa za vyakula kwakuwa hawaoni madhara yeyote pindi wanapotumia.

Sauti za Wananchi wakieleza kuhusu lewa wa matumizi ya bidhaa za vyakula vilivyyoisha muda wake.

Akizungumza kwa njia ya  Simu Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  Elizabeth Kakusa   amesema moja ya madhara ni  kupelekea  mtumiaji kupata homa na hata kuharisha kutokana na  sumu iliyopo ndani ya Chakula

Sauti ya Mratibu wa Elimu ya Afya kwa uma Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  Elizabeth Kakusa.

Katika hatua nyingine amebainisha  kuwa  wanafanya ukaguzi wa Vyakula sehemu mbalimbali kama vile  Madukani, na Viwandani ili kuhakikisha usalama wa bidhaa za Vyakula .