Mpanda FM

TBS yateketeza bidhaa feki

18 June 2026, 12:21 pm

Bidhaa zilizoteketezwa. Picha na Ben Gadau

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kanda ya magharibi limeteketeza bidhaa feki na bidhaa zisizokidhi viwango zilizokamatwa katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Na Ben Gadau -Katavi

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, afisa mdhibiti ubora kutoka TBS Kanda ya magharibi, Ezekiel Mubito, amewasihi wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kuzingatia miongozo na taratibu zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuhakikisha bidhaa zinazowafikia wananchi ni salama na zenye ubora unaokubalika.

Amewasihi wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kuzingatia miongozo na taratibu zinazotolewa na mamlaka hiyo

Amesema kuendelea kuuza bidhaa zisizokidhi viwango ni hatari kwa afya ya walaji na kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Sauti ya afisa mdhibiti ubora kutoka TBS Kanda ya magharibi, Ezekiel Mubito

Kwa upande wake, afisa afya wa manispaa ya Mpanda ambaye pia ni mratibu wa TBS katika manispaa hiyo, Erick Kisaka, amewataka wananchi kuepuka matumizi ya bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi, akieleza kuwa zinaweza kusababisha madhara mbalimbali ya kiafya kwa watumiaji.

Sauti ya afisa afya wa manispaa ya Mpanda ambaye pia ni mratibu wa TBS katika manispaa hiyo, Erick Kisaka

Zoezi hilo ni sehemu ya operesheni zinazoendelea kufanywa na TBS, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.