Mpanda FM

Wanawake washauriwa kuzingatia kanuni za unyonyeshaji

26 September 2023, 4:07 pm

Mama akinyonyesha, Picha na Mtandao

Wanawake wazingatie kanuni za unyonyeshaji ili kuwalinda Watoto na magojwa yasio ya kuambukizwa.

Na Gladness Richard – Mpanda

Wanawake wanaonyonyesha watoto manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kuzingatia kanuni za unyonyeshaji ili kuwalinda watoto na magojwa yasiyo ya kuambukizwa.

Maziwa ya mama ni kinga dhidi ya magojwa kwa mtoto.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Lishe Manispaa ya Mpanda Mwanaidi Salimu alipokuwa akizungumza na Mpanda Radio Fm amesema kuwa maziwa ya mama ni kinga dhidi ya magojwa kwa mtoto.

Sauti ya Afisa Lishe Manispaa ya Mpanda Mwanaidi Salimu

Kwa upande wao wananchi wamesema maziwa ya mama yanamsaidia mtoto kukua vizuri huku wakiwashauri wanawake wanaonyonyesha wawanyonyeshe watoto wao vizuri.

Sauti za wananchi

Kwa mujibu wa wataalam wa afya mtoto asiponyonyeshwa maziwa ya mama anashambuliwa na magonjwa mbalimbali huku afya yake ikidhoofika.