Mpanda FM

Pinda: Wazee zungumzeni na vijana

8 November 2023, 2:48 pm

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne wa  Tanzania Mizengo Peter Pinda akizungumza na wazee. Picha na Maktaba

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Peter Pinda metoa wito kwa wazee mkoani  Katavi kuwaelekeza vijana maadili mema katika jamii.

Na John Benjamin – Mpanda

Waziri Mkuu mtaafu wa awamu nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ametoa wito kwa wazee wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kuwafundisha maadili mema vijana ili kutojihusisha na matukio ya kiharifu.

Pinda ameleeza  kumekuwepo na  matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa yakifanywa na vijana ambapo amesema kunapaswa kuwepo kwa mikutano ambayo itatumika wazee kutoa elimu namna wanavyopaswa kuishi kwa kufuata maadili mema .

Sauti ya Mizengo Pinda

 Baadhi ya wazee  wameonyeshwa kusikitishwa kwa baadhi ya vikundi vya vijana kufanya matukio ya uvunjifu wa amani ambapo wametaja sababu ya malezi kwa Watoto imekuwa ni sababu ya vijana kufanya vitendo hivyo

Sauti ya Wazee