Mpanda FM

DC Mpanda wekeni akiba ya chakula

7 July 2025, 7:42 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph. Picha na Samwel Mbugi

“Bei zimepanda niwaombe tukumbuke kuweka akiba ya chakula”

Na Samwel Mbugi

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewahimiza wananchi kutunza chakula hususani katika kipindi hiki cha mavuno ambapo inaonyesha bei ipo juu.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wajasiriamali katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda ambapo amesema kuwa kazi hiyo ya utunzaji wa chakula inapaswa kusimamiwa na akina mama katika familia zao.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Pia Jamila amewakumbusha wananchi wa wilaya ya Mpanda uwepo wa lishe duni na kuwataka akina mama ambao ndio wahanga wakuu kula vizuri ili kusaidia kuondoa changamoto ya udumavu kwa watoto wao.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko alizindua kampeni ya lishe bora ili kukabiliana na changamoto ya udumavu.