Mpanda FM

Afunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja

13 July 2023, 10:10 am

MPANDA

Athumani Juma Mohamed Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amefunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo.

Akizungumzia ndoa yake Yengayenga amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na maumivu aliyoyapata mwanzo ya kuachwa na mke mmoja aliyekuwa amemuoa.

Wanawake hao wamesema wamefurahi kufunga ndoa na wanaona jambo la kawaida ingawa mwanzo lilikuwa gumu hasa kwa mke mkubwa alipofikishiwa na mmewe huku mama mzazi wa Yengayenga akifurahishwa na kubariki ndoa ya mwanae.

Mashaka Nassoro Kakulukulu Sheikh mkuu wa mkoa wa Katavi amekiri kufungisha ndoa hiyo huku akidai imefuata taratibu zote za dini na ametofautisha muda katika kufungisha ndoa hiyo.

#mpandaradiofm97.0

#bakwata

#katavists