Mpanda FM

Familia yaishukuru mahakama mwili wa ndugu yao kutofukuliwa mkoani Katavi

9 May 2024, 7:30 pm

Merehemu Lwitiko Bukuku enzi za uhai wake

“tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika kesi ya kufukuliwa kwa kaburi ambalo mara ya kwanza iliamriwa lifukuliwe na marehemu azikwe upya.”

Na Samwel Mbugi-Katavi

Familia ya marehemu aliyefahamika kwa jina la Lwitiko Bukuku wameishukuru Mahakama kwa kutenda haki katika kesi  iliyofunguliwa na anayedhaniwa kuwa ni mke wa marehemu akidai mumewe alizikwa kwa imani ya dini ya Kikristo badala ya imani ya dini Kiislam.

Hayo yamesema na Kaka wa marehemu Edward Bukuku wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm kuwa wanaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika kesi ya kufukuliwa kwa kaburi ambalo mara ya kwanza iliamriwa lifukuliwe na marehem azikwe upya.

Sauti ya kaka wa Marehemu Edward Bukuku

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mnazimmoja Mussa Alfani amesema kuwa mahakama imetenda haki kwani baadhi ya wananchi walikuwa wanamtuhumu kuwa yupo upande mmoja .

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mnazimmoja

Hata hivyo mwenyekiti amewataka wananchi wa Mtaa wake kuwa na imani na serikali kwani wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mwanachi.