Mpanda FM

Zaidi ya Heka 6 za mahindi zafyekwa na serikali

16 December 2023, 5:23 pm

Jeshi la akiba wakifyeka mahindi katika eneo la Mpanda Hotel. Picha na Mwandishi Wetu

Kufuatia agizo la manispaa ya Mpanda ambalo linazuia  kulima mazao marefu katikati ya makazi ya watu zoezi la kufyeka mazao Kwa ambao walikaidi agizo hilolimeendelea.

Na Mwandishi wetu – Mpanda

Kufuatia agizo la manispaa ya Mpanda ambalo linazuia  kulima mazao marefu katikati ya makazi ya watu Wananchi mkoni katavi wamekuwa na maoni tofauti baada ya zoezi la kufyeka mazao Kwa ambao walikaidi agizo hilo.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wananchi hao wamesema kuwa maamuzi ya kufyeka mazao  hayo yamesaidia kuweka mazingira salama na kuweka usawa Kwa wale ambayo hawajalima na pia huku Kwa upande mwingine wakishauri kutoza faini Kwa waliofanya hivyo na si kukata mazao.

Sauti ya wananchi

Baadhi ya wakulima waliokatiwa mazao wamedai uhalali wa maeneo hayo kwa kuomba vibali katika serikali za mitaa na pia wamekuwa wakilima maeneo kwa muda mrefu huku wakiyawekea ulinzi dhidi ya uhalifu.

Sauti ya waathirika
Barua ya moja ya waathirika waliofyekewa mahindi. Picha na Mwandishi Wetu

Akizungumza kwa njia ya simu kaimu Afisa mazingira manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Geofrey Mbunda amesema kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu na wale wote ambao wana mazao kwenye maeneo ambayo yalikatazwa yatafyekwa kwa mujibu wa taarifa ya katazo iliyotolewa.

Sauti ya Geofrey Mbunda

December 13 jeshi la akiba lilipita maeneo ya msasani na Mpanda hotel na kufyeka mazao yote marefu ambayo yapo karibu na makazi ya watu kufuatia agizo linalokataza kulima mazao hayo ambayo yanadhaniwa kuwa sehemu ya kuficha wezi au vitu vilivyo ibiwa.