Mpanda FM

Mawasiliano kuimarika Katavi

10 July 2023, 10:33 am

MPANDA

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali inatarajia kujenga minara ya mawasiliano katika mkoa wa Katavi ili kuimarisha mawasiliano kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani humo.

Hayo amesema na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Katavi akiwa kwenye ziara ya kikazi ambapo ameainisha maeneo ambayo itajengwa minara hiyo ni katika kata za Kasasa, Majimoto, Bulamata, Ipwaga, Kasekese, Katumba na Uruwila.

Mhadisi Kundo ameeleza kuwa kujenga mnara wa mawasiliano moja gharama yake ni wastani wa fedha Mil 350 na serikali imeamua kuwekeza fedha hizo kwenye kujenga minara kwa sababu inatija.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa chini ya uchumi wa kidigitali (Digital Economy) serikali ilianzisha sheria namba 11 ya mwaka 2006 ya mfuko wa mawasiliano kwa wote.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi, Onesmo Buswelu amemwomba Naibu Waziri huyo uharakishwaji wa ujenzi minara ya mitandao ya simu mkoni humo kwani wamezindua huduma ya M-Mama kwa lengo la kusaidia wanawake wajawazito wanaopata changamoto pindi ya kujifungua kwa kukosa mtandao ya simu pindi wanapotaka kutoa taarifa kwa gari la wagonjwa.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayahabarimawasilianonateknolojiayahabari

#katavists