Ruwasa Katavi kuongeza ukusanyaji mapato kupitia mfumo mpya wa malipo
12 December 2023, 10:11 pm
Picha na Mtandao
Mfumo huo utasaidia katika ukusanyaji mapato kwa kuwa wateja watalipia bili za huduma ya maji kwa njia ya simu na fedha hizo kuingia katika mfumo wa malipo ya serikali.
Na Betord Benjamini- Katavi
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa Mkoa wa Katavi inatarajia kuongeza ukusanyaji wa Mapato kupitia huduma ya utoaji wa maji vijijini baada ya kuanza kutumia mfumo mpya wa malipo ya huduma ya maji kwa njia ya mtandao uliounganishwa na mfumo wa malipo ya serikali GPG.
Akizungumza wakati akifunga semina ya siku kumi kwa viongozi wa utoaji wa huduma ya maji ngazi jamii [CBWOSS] Meneja wa Ruwasa mkoa wa Katavi Mhandisi Peter Ngunula amesema kuwa mfumo huo utasaidia katika ukusanyaji mapato kwa kuwa wateja watalipia bili za huduma ya maji kwa njia ya simu na fedha hizo kuingia katika mfumo wa malipo ya serikali.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa wanatarajia kwenda kuongeza makusanyo kwenye [CBWOSS] baada ya mafunzo hayo ya kuwahudumia wateja kwa njia ya Mtandao katika kufanya malipo ya bili zao za maji.
Jumla ya mikoa sita nchini inayotoa huduma ya maji vijijini Ruwasa imeweza kuunganishwa na mfumo wa malipo ya serikali GPG ili kudhibiti upotevu wa makusanyo ya mapato hayo. Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Shinyanga, Mwanza, Katavi, Rukwa, Morogoro na Mwanza.