Mpanda FM

Wananchi Katavi waaswa kukata bima  ya afya

20 December 2023, 4:06 pm

Kufuatia uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote wananchi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kukata bima  ya afya.

Na Deus Daud – KATAVI

Kufuatia uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote wananchi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kukata bima  ya afya ili kusaidia kumudu gharama za matibabu pindi wanapopitia changamoto ya maradhi

Akizungumza na Mpanda Radio Fm Manager wa mfuko wa taifa wa bima ya afya [NHIF] kwa mkoa wa Katavi Ally Endrew Mwakababu amesema kuwa sheria inawataka wananchi wote kuwa na bima ya afya  hivyo ni muhimu kwa  kujiunga na mfuko wa bima ya afya.

Sauti ya Ally Mwakababu

Kwa upande wao wananchi wameeleza namna  walivyoipokea  sheria  mpya ya bima ya afya kwa wote iliyosainiwa hivi karibuni.

Sauti ya Wananchi

Sheria ya bima ya afya kwa wote imesainiwa mwanzoni mwa mwezi Desember na Rais wa Jamuhuri ya Muunganio wa Tanzania  Samia Suluhu Hassani kufuatia uwepo wa mswada wa sheria hiyo toka mwaka 2022.