Mpanda FM

Watoto wawili wa familia moja  wafariki kwa ajali ya moto Katavi

11 September 2023, 9:55 am

Wananchi pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi katika tukio la ajali ya moto Mtaa wa Tulieni. Picha na Site Tv

Katika eneo la tukio kimekutwa kiberiti ambacho kinadhaniwa kuachwa na mtu .

Na William Liwali-Katavi

Watoto wawili wa familia moja  Florida Froline   na Ferisian Froline wenye umri wa miaka mitatu wamefariki dunia  baada ya nyumba yao kuungua  moto mtaa wa Tulieni kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Shuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa watoto hao walikuwa ndani peke yao wakati moshi  mkubwa ulioambatana na moto kuonekana  katika nyumba hiyo.

Sauti ya Mashuhuda wa tukio hilo la ajali ya moto

Mwenyekiti wa mtaa wa Tulieni Hussein Kasomela amesema  baada  ya kupata taarifa   amefika eneo la tukio kwa ajili ya kushirikiana na wananchi kuwaokoa watoto waliokuwa wahanga wa mkasa huo.

Sauti Ya Mwenyekiti wa Mtaa Tulieni Hussein Kasomela

Mkuu wa kitengo cha oparesheni kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya  Mpanda Inspekta Geofrey Goerge Mwambungu amesema katika eneo la tukio wamekuta kiberiti ambacho kinadhaniwa kuachwa na mtu anayedhaniwa kufanya tukio hilo huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini katika uangalizi wa watoto.

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha oparesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Mpanda Geofrey Mwambungu

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani amefika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo .

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani