Mpanda FM

Akutwa amejinyonga hadi kufa kwa kipande cha chandarua

22 June 2026, 11:12 am

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi kamishna msaidizi mwandamizi Kaster Ngonyani.

Tumeshtushwa na tukio hili na huyu kijana hatumfahamu.

Na Anna Milanzi Katavi

Kijana mmoja wa kiume ambaye bado hajafahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha chandarua katika mtaa wa Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Kaster ngonyani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema taarifa ziliwafikia kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa huo.

Sauti ya Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi kamishna msaidizi mwandamizi Kaster Ngonyani

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Nsemulwa Emili Kilomo amewaomba wakazi wa mtaa huo pindi wanapopata shida waeleze ili waweze kusaidiwa.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Nsemulwa Emili Kilomo

Wakazi wa mtaa huo Anastanzia Maembe, John Manyanza pamoja na balozi wa shina namba sita Shabani Milambo eneo ambalo tukio limetokea  wameshtushwa na tukio hilo na kueleza kuwa kijana huyo hawamfahamu.  

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Nsemulwa na maeneo jirani waliokimbilia tukio hilo.picha na Anna Milanzi
Sauti ya mashuhuda.

   Kutokana na tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ametoa rai kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na kueleza kuwa changamoto zinapojitokeza ni vizuri  kuzungumza na wazee,viongozi wa dini  na kumwamini Mungu.