Mpanda FM

Wadau wa Maendeleo Washauri Utunzaji wa Mazingira

9 August 2023, 6:24 am

MPANDA

Wadau wa maendeleo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameuomba uongozi wa manispaa ya Mpanda kutunza mazingira ya msitu uliopo eneo La uwanja wa azimio pamoja na kuimarisha miundombinu ya barabara inayoingia hospitali ya manispaa.

Wameyasema hayo katika kikao cha wadau wa maendeleo ambapo wamesema shughuli za kibinadamu ambazo zinaendelea katika eneo hilo ni vyema zikasitishwa ili kutunza eneo hilo pamoja na kukarabati barabara inayoingia hospitali ya manispaa ambayo imechakaa.

Akijibia hoja ya upanuzi wa barabara kuingia katika geti la hospitali ya manispaa meneja wa TARURA amesema kuwa katika mwaka mpya wa bajeti wa serikali wamepanga kukarabati barabara hiyo,pamoja na barabara zingine.

Kwa upande wa utunzaji msitu katika eneo la uwanja wa azimio kaimu mkurugenzi manispaa ya mpanda amesema kuwa hatua za awali zimeshachukuliwa ikiwemo kuondoa mtu aliekuwa anafanya shughuli katika eneo hilo na taratibu za kuutunza zaidi zitaendelea.

#mpandaradiofm97.0

#ccmtanzania