Mpanda FM

Migogoro ya Ndoa ,Wivu  wa Kimapenzi Chanzo cha Matukio ya Ukatili Katavi

3 April 2024, 9:26 pm

picha na Mtandao

” Wanandoa wanapaswa kusuluhisha Migogoro  ya ndoa kwa njia ya amani  na kuripoti vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa  katika mamlaka husika

Na Lilian Vicent -Katavi

Hayo yameelezwa na Afisa Ustawi wa Jamii  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumiye Longo  wakati akizungumza na Mpanda Redio Fm na kuongeza kuwa Wanawake na Watoto  ndio Wahanga wakubwa wa Matukio hayo

Imeelezwa kuwa  Migogoro ya Ndoa na Wivu  wa kimapenzi ni moja ya sababu zinazopelekea kuongezeka kwa matukio ya Mauaji  katika jamii.

Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumiye Longo 

Katika hatua nyingine amewataka  Wanandoa kusuluhisha Migogoro  ya ndoa kwa njia ya amani  na kuripoti vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa  katika mamlaka husika.

Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumiye Longo akiwahasa wanandoa kuripoti matukio ya ukatili

Kwa  upande wao Wananchi  wameeleza  kuwa  wivu   wa kimapenzi  na usaliti unapelekea    kuibuka kwa  matukio hayo.

Sauti za wananchi wakitoa maoni Mseto juu ya sababu za matukio ya ukatili na mauaji katika jamii

Jamii imeaswa kutoa taarifa za Matukio kama hayo kwa haraka ili kuthibiti kutokea kwa matendo hayo .