Mpanda FM
Mpanda FM
24 April 2026, 10:38 am

“Niwasihi wananchi wazae watoto watakaoweza kuwahudumia”
Na Anna Mhina
Katika jitihada za kupunguza ongezeko la vitendo vya uhalifu jamii imetakiwa kuzingatia umuhimu wa malezi bora ya watoto watakaokuwa raia wema na wenye mchango chanya katika familia na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Inspekta Kelvin Fuime polisi kata ya Kawajense ofisi ya OCD Mpanda alipokuwa akizungumza na Mpanda radio FM na kuiasa jamii kuzaa watoto watakaoweza kuwahudumia.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini akiwemo sheikh mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Nassoro Kakulukulu na askofu wa makania ya Tanzania Assemblies of God ( TAG) Katavi Anjello Kachele wamesema ni kosa kuzaa watoto ambao huna uwezo wa kuwapa mahitaji muhimu.
Kuhudumia watoto ni jukumu la msingi lenye umuhimu wa kujenga afya bora ya kimwili na kiakili kuhakikisha usalama na kuwaandaa kuwa raia wema na wenye tija.