Mpanda FM

Mwanaume akutwa amenyongwa na mwili wake kutupwa Katavi

4 April 2024, 4:28 pm

Picha na Mtandao

Baada ya polisi kuuchukua Mwili wa Marehemu kikosi cha ulinzi na usalama kilirudi tena kufanya Misako ya Watu wanaokunywa Pombe Saa za Kazi

Na Samwel Mbugi-Katavi

Mtu mmoja anaekadiriwa kuwa na  Umri kati ya Miaka 40-45 amekutwa amenyongwa na Mwili wake kutupwa maeneo ya Relini Mtaa wa Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo Selestino  Shauritanga wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm na amesema kuwa amefika eneo la tukio na kufanikiwa kuutambua Mwili wa Marehemu huyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli Selestino  Shauritanga akielezea tukio hilo

Pia shauritanga amesema kuwa baada ya Polisi kuuchukua Mwili wa Marehemu kikosi cha Ulinzi na Usalama kilirudi tena kufanya Misako ya Watu wanaokunywa Pombe Saa za kazi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli Selestino  Shauritanga akielezea tukio hilo

Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wamefanya msako  kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema.

This image has an empty alt attribute; its file name is ngonyani.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani  amethibitisha kutokea kwa tukio .Picha na Gladness Richard

Sauti Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani  akithibitisha kutokea kwa tukio