Wananchi Katavi watakiwa kuchukua vitambulisho vya taifa
4 April 2024, 8:45 pm
Afisa Msajili mamlaka ya vitambulisho vya taifa wilaya ya Mpanda Mauna Karumbeta akiwa katika Studio za Mpanda Redio Fm .Picha na Anna Milanzi
Amewataka wananchi kuthamini juhudi za serikali kwa kufika kuchukua vitambulisho na kuvitunza kwani serikali imetumia gharama“
Na Lilian Vicent -Katavi
Wito umetolewa kwa Wananchi wa mkoa wa Katavi ambao hawakupata Vitambulisho vya NIDA kufika Ofisi za Mitaa Wanayoishi ili kuweza kuvichukua kabla havijarudishwa Ofisi za NIDA .
Hayo yamesemwa na Afisa Msajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Mpanda Mauna Karumbeta Wakati akizungumza na Mpanda Redio Fm na kueleza kuwa kuna baadhi ya Kata Vitambulisho vya awamu ya kwanza bado vipo mpaka sasa Wananchi hawajavichukua.
Sauti ya Afisa Msajili mamlaka ya vitambulisho vya taifa wilaya ya Mpanda Mauna Karumbeta
Nae Afisa usajili Tanganyika Zainabu Mwinyimvua amewataka wananchi kuthamini juhudi za serikali kwa kufika kuchukua vitambulisho na kuvitunza kwani Serikali imetumia gharama.
Sauti ya Afisa usajili Tanganyika Zainabu Mwinyimvua
Afisa usajili Tanganyika Zainabu Mwinyimvua akiwa katika Studio za Mpanda Redio Fm .Picha na Anna Milanzi
Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia kwani wamesubiri kwa muda mrefu na ili wakwamisha kupata baadhi ya huduma zinazohitaji vitambulisho.
Sauti za Wananchi Mkoani Katavi wakishukuru kuletewa vitambulisho hivyo