Mpanda FM

Madiwani Tanganyika waomba mafunzo ya hewa ya Ukaa

4 September 2023, 9:46 am

TANGANYIKA

Ili Kuitambua biashara ya hewa ya ukaa Madiwani wilaya ya Tanganyika wameitaka Halmashauri hiyo kuwapa madiwani Mafunzo ya biashara ya hewa ya ukaa.

Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka Wamesema katika vikao vilivyopita wameomba kupewa mafunzo ya biashara hiyo lakini bado halijatekelezwa licha ya kunufaika ya pesa za hewa ukaa lakini hawajui namna pesa inavopatikana.

Kwa upande wake Afisa Maliasili na Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bruno Nichoulaus Mwaisaka Amesema awali mafunzo yalishindikana kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha kuahidi kutolewa kwa mafunzo siku za hivi Karibuni.

Biashara Ya hewa ukaa imeanza baada ya vijiji 8 kuwekwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi wa wananchi kujipangia namna ya kutumia ardhi kwa faida yao huku imetajwa moja ya Malengo ya mradi ni kuhifadhi misitu ya asili na mazingira, kulinda na kuhifadhi bionuai zote muhimu hasa zilizo hatarini kutoweka

#mpandaradiofm97.0