Mpanda FM

Mbunge Kakoso awakataa madereva walevi

21 November 2023, 10:34 pm

Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini akiwa ndani ya gari mpya la wagonjwa. Picha na Anna Milanzi

Mbunge Kakoso ameshauri halmashauri hiyo kufanya marekebisho ya magari yaliyoharibika ili yaweze kuendelea kutoa huduma.

Na Anna Milanzi -Katavi

Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini mkoani Katavi amekabidhi gari mpya ya wagonjwa  kwa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika huku akisisitiza kuajiri madereva walio na weledi katika kazi.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi gari hilo la wagonjwa mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso amemwomba mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema gari hilo ikiwemo kuajiri madereva wasio walevi.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso akizungumza na wananchi . Picha na Anna Milanzi

Kadhalika na hilo Mbunge Kakoso ameshauri halmashauri hiyo kufanya marekebisho ya magari yaliyoharibika ili yaweze kuendelea kutoa huduma.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini

Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo wakishuhudia Makabidhiano ya Gari hiyo ya Wagonjwa.Picha na Anna Milanzi

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Shaban Juma  wakati akikabidhiwa Gari hiyo ameishukuru Serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwapatia Gari hiyo na kuahidi kumpatia Dereva Makini .

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika

Mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika Shaban Juma akizungumza ,huku upande wa kushoto ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Tanganyika Alex Mrema na Upande wa kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini

Mkuu wa Wilaya hiyo Onesmo Buswelu kupitia Vyombo vya Usalama  ameahidi kufuatilia Madereva wasiozingatia weledi katika kazi zao.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Ya Tanganyika

Wananchi wa wilaya ya Tanganyika wakishuhudia Gari Mpya ya Wagonjwa iliyokabidhiwa katika halmashauri hiyo.Picha na Anna Milanzi