Mpanda FM
Mpanda FM
4 May 2026, 6:36 pm

“Nitoe rai msipende kupambana na tukio la moto wenyewe”
Na Roda Elias
Jeshi la zimamoto mkoani Katavi limetoa elimu kwa wananchi kuhusiana na majanga yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha, kwa baadhi ya maeneo na majanga ya moto yanayotokana na ajali.
Hayo yamejiri kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya zimamoto duniani, maeneo ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Lilian Wanna, kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto mkoani Katavi amesema kuwa jamii haipaswi kujichukulia maamuzi ya kupambana na majanga hususani majanga ya moto badala yake wanapaswa kutoa taarifa kwa jeshi hilo ili kufanikisha uokozi.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi waliohudhuria katika utolewaji wa elimu hiyo wameeleza namna ambavyo wameipokea elimu hiyo huku wakiliomba jeshi hilo kuendelea kutoa elimu hiyo mara kwa mara.
Siku ya zimamoto duniani huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 4 mwezi wa 5 ambapo mwaka huu mkoani katavi jeshi hilo limedhimisha kwa kufanya matembezi kwa baadhi ya maeneo katika manispaa ya Mpanda.