Mpanda FM

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi afuturisha

8 April 2024, 12:33 pm

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi.Picha na Mtandao

viongozi wa serikali na wasio waserikali wamekuwa na mchango katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani  katika dhehabu hilo kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kufuturisha”

Na Deus Daudi-Katavi

Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi amefanya hafla ya kufuturisha Waumini na wasio Waumini wa dini ya Kiislamu katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi

Akizungumza wakati wa hafla Hiyo Katibu wa baraza la Waislam mkoa wa Katavi (BAKWATA) Omary Muna amesema kuwa Viongozi wa Serikali na wasio wa Serikali wamekuwa na Mchango katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  katika Dini hiyo kwa kutoa Misaada Mbalimbali ikiwemo kufuturisha.

Sauti ya Katibu wa Baraza la Waislam Mkoa wa Katavi { BAKWATA} Omary Muna akizungumza

Kwa upande wake Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Nassoro Kakulukulu  ameendelea kutoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda kwa kuandaa hafla hiyo .

Sauti ya Shehe mkuu wa mkoa wa katavi Nassoro Kakulukulu akizungumza

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Nassoro Kakulukulu.Picha na Mtandao

Hafla hiyo  imewakutanisha watu kutoka Sekta  tofauti Kama madereva bodaboda, bajaji pamoja na wafanya biashara , waumini na wasio waumini wa dini ya Kiislam  manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.