Mpanda FM

Baraza la madiwani Mpanda lapitia bajeti ya fedha

28 September 2023, 11:29 pm

Baadhi ya Madiwani wakisikiliza kikao cha mapitio ya bajeti ya fedha kwa mwaka 2022 – 2023. Picha na Maktaba

Baraza la Madiwani Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wafanya kikao kifupi cha mapitio ya bajeti ya fedha kwa mwaka 2022 – 2023.

Na Mwandishi wetu – Mpanda
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limefanya kikao kifupi cha mapitio ya bajeti ya fedha kwa mwisho wa mwaka 2022 – 2023.

Akisoma Taarifa hiyo Paskola Mzinga Mkuu wa Idara ya Fedha amesema kikao hicho ni muhimu na na kipo kisheria huku akiwataka madiwani hao kuendelea kushikamana katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Fedha Paskola Mzinga

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akizungumza katika kikao hicho amewataka madiwani kupitia bajeti hiyo kutekeleza kwa weredi miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata zao ndani ya Manispaa ya Mpanda.

Sauti ya Mstahiki Meya Haidary Sumry