Mpanda FM

Wananchi Kilimani waneemeka ufugaji samaki

16 June 2023, 7:24 pm

MPANDA

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kilimani kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamekuwa na maoni mseto kutokana na fursa za ufugaji wa samaki zinazofanywa na mwekezaji Injinia Ismail Nassoro.

Wakizungumza na kituo hiki wananchi wamesema kupitia fursa hiyo ya ufugaji wa samaki wamekuwa wakijipatia kitoweo sambamba na fursa za kujiingizia kipato kutokana na ufugaji huo.

Kwa upande wake Injinia Ismail Nassoro akizungumza katika kipindi cha kumekucha Tanzania amesema ukata na uhaba wa mitaji imekuwa ni kikwazo kwa baadhi ya wananchi kushindwa kufikia ndoto zao hasa katika fursa za uwekezaji na kuwashauri kuthubutu kuwekeza kwa kuanzia na mitaji midogo.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayamifugonauvuvi

#katavists