Mpanda FM

Martha Achangia Milion 5 Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto

26 July 2023, 5:57 pm

NSIMBO

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi, Martha Mariki amekabidhi hundi ya Shilingi Milioni Tano kwaajili ya kusaidia ukarabati wa Jengo la Mama na Mtoto Katika Kijiji Cha Kajeje Kata ya Kanoge Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.

Mbunge Martha Mariki amesema kwa kutambua Juhudi zinazofanywa na serikali katika kuimarisha miundombinu ya Afya katika Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Nsimbo kwa ujumla na kuchangia Milioni Tano ili kuharakisha ukarabati Jengo la Mama na Mtoto.

Ameeleza kuwa miongoni mwa Mambo ambayo serikali imekuwa ikiyafanya katika mkoa wa Katavi nikuendelea kujenga Zahanati,Vituo vya Afya ,Hospitali za Wilaya pamoja na uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo imeanza kufanya kazi na kuwaepushia adha wananchi kwenda kutibiwa katika Mikoa mingine.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa amemshukuru Mbunge Martha Mariki kwa Mchango wake na Ameainisha kuwa halmashauri wametenga Milioni Hamsini kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la mama na Mtoto katika Kijiji cha Kajeje.

#mpandaradiofm97.0

#CCM