Mpanda FM

AJINYONGA BAADA YA KUMJERUHI MUMEWE

30/03/2022, 1:16 PM

KATAVI. 

Mkazi wa kitongoji cha Kamlenga, Kijiji cha Sibwesa wilayani Tanganyika, Mande Emanuel (30) amejinyonga baada ya kumjeruhi mumewe, Dotto Enos (35) kwa kumkata mapanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame
Sauti ya kamanda Ally Makame

Aidha Kamanda Makame amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo kwani mwanamke alikuwa hataki kwenda shamba kulima hali iliyopelekea kutokea ugomvi huo.

Sauti ya Kamanda Makame

Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO) takribani watu 800,000hufariki kwa kujitoa uhai kila mwaka na kuwa matukio hayo ni mengi hasa kwa vijana wa umri kati ya miaka 10 hadi 25 katika mataifa yenye kipato cha chini.