Mpanda FM

MPANDA, Wananchi Walia na Ubovu wa Barabara

24 January 2024, 2:57 pm

Wananchi Wamesema Barabara nyingi zilizopo Manisapa zina Mashimo yaliyojaa maji na matope, mitalo iliyojaa michanga na takataka inayosababisha maji kuchepuka na kuingia barabaraniPicha Na Festo Kinyogoto

Na Gladness Richard-katavi

Wananchi  wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara kutokana na changamoto wanazopitia hasa kipindi hiki cha mvua.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm Wananchi wamesema barabara nyingi zilizopo Manisapa zina Mashimo yaliyojaa maji na matope, mitalo iliyojaa michanga na takataka inayosababisha maji kuchepuka na kuingia barabarani, Jambo linalosababisha vyombo vya usafiri kuharibika na kutofika baadhi ya maeneo, Hivyo wameziomba mamlaka husika kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ya Barabara.

Sauti za wananchi wa Manispaa ya Mpanda wakieleza changamoto wanazopitia kutokana na ubovu wa barabara

Moja ya barabara inayopatikana kata ya makanyagio Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ikiwa katika hali isiyoridhisha. Picha na Festo Kinyogoto.

Barabara inayopatikana kata ya Irembo Manispaa ya Mpanda ikiwa katika hali isiyoridhisha. Picha na Festo Kinyogoto

Meneja wa TARURA Manispaa ya Mpanda Mhandisi Kahoza Joseph, amekiri kuwepo kwa changamoto kwenye baadhi ya barabara za Manispaa na wao kama mamlaka Husika wamejipanga kutengeneza  Barabara zote za ndani ya Manispaa na kuna maeneo mengine mkandarasi yupo kazini .

Sauti ya Mhandisi akieleza juu ya hali ya barabara na mikakati iliyopo kutatua changamoto hiyo

Kahoza ameongezea kwa kuwaomba Wananchi kutokutupa takataka kwenye Mifereji kwani husababisha mitalo kiziba, na mvua zinaponyesha husababisha Maji kutuama na kupelea uharibifu wa Miundombinu ya Barabara.