Mpanda FM

Wananchi Katavi wanaelewa nini kuhusu ugonjwa wa macho mekundu?

18 January 2024, 12:50 am

Picha na Mtandao

Ugonjwa huo unawapata watu wa rika zote hivyo jamii inapaswa kupata Matibabu mapema iwezekanavyo mara tu watakapoona viashiria vya Ugonjwa huo.

Na Gladness Richard-Katavi

Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameeleza namna wanavyoufahamu Ugonjwa wa Macho Mekundu( Red eyes)

Wakizungumza na Mpanda Redio Fm Wananchi hao wamesema kuwa Mtu anaepata Ugonjwa huo Macho yanavimba na kuwa Mekundu huku Wananchi wengine wakiwa hawana uelewa dhidi ya Ugonjwa huo

Sauti za Wananchi wakieleza namna wanavyouelewa ugonjwa wa Macho mekundu (Red Eyes)

Kwa upande wake Daktari wa Macho kutoka katika kituo cha afya cha St.Aloyce Jackson Noel ameeleza sababu hasa za ugonjwa huo na kupelekea macho kuwa Mekundu.

Sauti ya Daktari wa Macho kutoka katika kituo cha afya cha St.Aloyce Jackson Noel akieleza sababu za ugonjwa huo

Jackson ameongeza kwa kusema kuwa Ugonjwa huo unawapata watu wa rika zote hivyo jamii inapaswa kupata Matibabu mapema iwezekanavyo mara tu watakapoona viashiria vya Ugonjwa huo.

Wizara ya afya imewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Macho Mekundu (Red eyes) Maambukizi ya Kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” iliyoibuka nchini hivi karibuni.

Dalili ya ugonjwa huo ni pamoja na macho kuwasha, kuchomachoma, kuuma, macho kutoa machozi na kutoa tongo tongo za njano.