Mpanda FM

Wazazi, walezi Katavi washauriwa kuchukua tahadhari kipindi cha mvua

18 December 2023, 3:46 pm

Wazazi na walezi mkoani Katavi, washauriwa kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua  kwa kuwalinda Watoto.

Na Gladness Richard – KATAVI

Wazazi na walezi mkoani Katavi wameshauriwa kuendelea kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua  kwa kuwalinda watoto  wasicheze pembezeno mwa mito.

Wakizungumza na Mpanda radio  fm   wakati wakitoa maoni kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na baadhi ya watoto kuonekana maeneo hatarishi wananchi wamesema kuwa kila mzazi anatakiwa kuwa mwangalizi  wa karibu kwa mtoto wake ili kuepusha majanga.

Sauti ya Wananchi

 Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi Geofrey Mwambungu amesema kuwa Wazazi wanatakiwa kuhakikisha Watoto wanakuwa sehemu salama pamoja na kuchukua tahadhari zote ili kuwakinga na majanga yanayoweza kujitokeza katika msimu  huu wa mvua.

Sauti ya Geofrey Mwambungu

Mwambungu ameongeza kwa kusema kuwa  wananchi wanapaswa kufunika mashimo  ya vyoo ambayo hayajafunikwa ili kuepusha ajali kwa Watoto.