Mpanda FM

Wananchi washauriwa kutumia wiki ya maadhimisho ya usafishaji duniani kufanya usafi

14 September 2023, 6:30 pm

Watu wakifanya usafi. Picha na Mwananchi

Maadhimisho ya usafishaji duniani hufanyika kila ifikapo September 16 ya kila mwaka kwa lengo la kuikumnusha jamii juu ya umhimu wa usafi wa mazingira

Na Veronica Mabwile – Mpanda

Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameshauriwa kuitumia wiki ya maadhimisho ya usafishaji duniani kufanya usafi katika maeneo yao ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali.

usafi wa mazingira ni nyenzo muhimu ya kuyaondoa magonjwa katika jamii

Wito huo umetolewa na afisa Afya Manispaa ya Mpanda Erick Kisaka wakati akiongea na kituo hiki kuelekea kilele cha usafishaji duniani ambacho hufanyika kila mwaka September 16 na kusema kuwa usafi wa mazingira ni nyenzo muhimu ya kuyaondoa magonjwa katika jamii

Sauti ya Afisa Afya Manispaa ya Mpanda Erick Kisaka

Kwaupande wao baadhi ya wakazi wa manispaa ya Mpanda wakiongea na kituo hiki juu ya zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo yao wamelelamikia upungufu wa vitendea kazi yakiwemo magari kwa ajili ya kuzolea takataka jambo ambalo wamesema linakwamisha zoezi hilo kutokufanyika ipasavyo

Sauti ya wananchi wakizungumza kuhusu zoezi la usafi

Maadhimisho ya usafishaji duniani hufanyika kila ifikapo September 16 ya kila mwaka kwa lengo la kuikumnusha jamii juu ya umhimu wa usafi wa mazingira na kuomgeza uelewa juu ya mambo yahusuyo usafi wa mazingira