Mpanda FM

Wakazi wa Ibindi Walia na Barabara

20 January 2023, 4:11 am

NSIMBO

Wananchi wa kijiji cha ibindi kata ya Ibindi Halmshauri ya Nsimbo  Mkoani Katavi wameuomba uongozi wa kata hiyo kuboresha miundombinu ya barabara ambayo wametaja kama kikwazo katika shughuli za kimaendeleo.

Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi hao wamesema barabara kutoka Magula,Ibindi kuelekea Kashelami sio rafiki kutokana na kukatika pamoja na madaraja kujaa Maji huku wakisema imekuwa ikikwamisha shughuli za kimaendeleo ya kukuza uchumi za kila siku.

Aidha kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Ibindi Peter Ntangwa amekiri kuwepo kwa changamoto huku akisema  tayari wataalamu wamefika kwa ajili ya kufanya tathmini na amewataka wananchi kuvumilia katika kipindi hiki ambacho serikali inashughulikia suala hilo