Mpanda FM

Ng’ombe 14 wafa baada ya kunywa maji yenye sumu

20 December 2023, 5:05 pm

Baadhi ya Ng’ombe waliokufa baada ya kunywa maji yanayosadikiwa kuwa na sumu. Picha na Betold Chove

Ng’ombe 14 wamekufa baada ya kusadikika kunywa maji yenye sumu katika kitongoji cha Mwenge.

Na Ben Gadau – Katavi

Ng’ombe 14 wamekufa baada ya kusadikika kunywa maji yenye sumu katika kitongoji cha Mwenge kijiji cha Sosaiti kata ya Magamba Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Nimeagiza wataalamu kwa ajili ya kufuatilia jambo hili na mchakato wa kulipwa fidia kwa mfugaji huyo zitafanyika.

Akizungumza na Mpanda Radio Fm Masele Sitta mkazi wa Kitongoji cha Njiapanda ambaye ni mmiliki wa Ng’ombe hizo amesema mifugo yake imekufa mara baada ya kunywa maji yanayodhaniwa kuwa na sumu katika eneo hilo.

Sauti ya Masele Sitta

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa wameiomba serikali kuyafanyia vipimo maji hayo yanayodhaniwa kuwa na sumu ili kuepusha adha ya mifugo kufa kutokana na maji hayo.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kufuatia changamoto hiyo ya Ng’ombe hao kufa tayari ameagiza wataalamu kwa ajili ya kufuatilia jambo hilo huku akisema kuwa mchakato wa kulipwa fidia kwa mfugaji huyo zitafanyika.

Sauti ya Jamila Yusuph