Mpanda FM

Kusuasua mradi wa machinjio Mzanda awa mbogo

3 March 2026, 5:03 pm

Mwenyekiti Mzanda akitoa maelekezo kwa mtendaji wa mtaa. Picha na Samwel Mbugi

“Tumuombe mkurugenzi autoe mradi huu kwenye kata”

Na Samwel Mbugi

Mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda hotel Ibrahim Msanda amefanya ziara ya ukaguzi wa marekebisho ya miundombinu ya mradi wa machinjio ya mkoa wa Katavi iliyopo kata ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda.

Akizungumza mbele ya watumishi wa machinjio hiyo amemuelekeza mtendaji wa mtaa huo kumuandikia barua mkurugezi wa manispaa ya Mpanda kuutoa mradi ngazi ya kata na kuurudisha ngazi ya mtaa, baada ya kuona changamoto ambazo ni uzembe katika kufuatilia mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

Sauti ya mwenyekiti

Kupitia ziara hiyo Msanda amesema millioni 14 zimewekwa kwenye account ya kata lakini hakuna kinachoendelea jambo linasababisha kusuasua kwa mradi ambao upo kwenye mtaa anaousimamia.