Mpanda FM
Mpanda FM
18 May 2026, 5:57 pm

“Tunashinikiza serikali imuachie Tundu Lissu”
Na Leah Kamala
Wananchi kata ya Kakese manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamepongeza hatua ya kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara kwa CHADEMA katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa Katiba mpya.
Hayo yamejiri katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika katika uwanja wa Mkwajuni uliopo kata ya Kakese ambapo wananchi wamesema serikali inapaswa kuhakikisha mchakato cha Katiba mpya unatekelezwa katika kuimarisha demokrasia na ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya kisiasa.
Akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa chadema mkoa wa Katavi Rhoda Edward Kunchelaamesema kuwa wananchi wanasubiri kuona mchakato wa Katiba mpya ili kutoa fursa ya maboresho na haki za wananchi.
Kwa upande wake katibu wa chadema manispaa ya Mpanda Iddy Faraji amesema kuwa chama hicho kinaendelea kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao za msingi kwa njia ya amani na utulivu.