Mpanda FM

Maabara yajengwa Katavi kutatua kero zinazowakabili akinamama wa kiisilam

1 April 2024, 9:16 pm

Jengo la Maabara inayojengwa .Picha na Mtandao

Akinamama wa kiislamu wamefurahishwa na uanzishwaji wa maabara hiyo huku wakidai itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto zinazowakabili kwani watapatiwa huduma na wataalam wa kike na si wa kiume kama ilivyo sasa.

Na Betold Chove -Katavi

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Katavi wamefanikisha zoezi la ujenzi wa Maabara ili kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili Kinamama wa kiislamu pindi wanapokwenda kupata huduma za Matibabu katika vituo vingine na kupatiwa huduma na wataalamu wa Kiume.

Shekh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu amesema mbali na kutatua changamoto bali  ni moja ya kuiunga mkono kwa Serikali kuboresha huduma za afya huku Katibu wa BAKWATA Omary Muna akieleza Maabara hiyo inajengwa kwa michango ya wadau na waumini wa dini hiyo.

Sauti ya Shekh Mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu

Shekh Mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu .Picha na Mtandao

Kwa upande wao kinamama wa kiislamu wamefurahishwa na uanzishwaji wa Maabara hiyo huku wakidai itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto zinazowakabili kwani watapatiwa huduma na wataalamu wa kike sio wakiume kama ilivyosasa.

Sauti ya Kinamama wa Kiislamu wakizungumza juu ya uanzishwaji wa Maabara hiyo

Katika hatua nyingine wadau wengine wameombwa kujitokeza kuunga mkono ujenzi huo kwa kutoa Michango  ili kukamilisha ujenzi wa Maabara hiyo.