Mpanda FM

Machinga Katavi walia na kampuni za utoaji mikopo isiyozingatia sheria

21 November 2023, 8:33 pm

Picha na Mtandao

Baadhi ya kampuni hizo zinatoa mikopo kwa kutofuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Na John Benjamini-Katavi

Wafanyabiashara wadogo [machinga]  mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuzifuatilia kampuni ambazo zinajihusisha na utoaji wa mikopo kwa wafanyabiashara kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya udanganyifu pamoja na kutoa mikopo yenye lengo la kuwakandamiza.

Hayo yamesemwa katika kikao kilichofanywa na wamachinga mkoa wa Katavi na kueleza kuwa baadhi ya kampuni hizo zinatoa mikopo kwa kutofuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

Sauti ya wafanyabiashara Wadogo (Machinga)

Kwa upande wake mwenyekiti wa machinga wilaya ya Mpanda Haji Mponda amesema licha ya changamoto hiyo lakini awali walikua wakikabaliwa na changamoto ya viongozi ngazi ya serikali kutowashirikisha wamachinga hao katika maamuzi pindi Masoko yanapoanzishwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Machinga Wilaya Ya Mpanda

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema  Serikali imeweka Mazingira Mazuri kwa Machinga kufanya kazi baada ya kuona wakisumbuliwa katika biashara zao.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi Jamila Yusuph .Picha na Mtandao

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda