Mpanda FM

Wananchi Waaswa Kuzingatia Usafi Kipindi cha Mvua

17 January 2023, 5:42 pm

MPANDA
Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameshauriwa kuzingatia kanuni za usafi kipindi hiki cha masika ambapo mvua zinaendelea kunyesha ili kujiepusha na magojwa ya mlipuko.

Wakizungumza na mpanda radio fm wakazi wa manispaa ya mpanda wamesema ipo tabia kwa baadhi ya watu wanatiririsha kinyesi kutoka katika vyoo vyao pindi mvua inaponyesha na kuomba hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wake mganga mkuu mansipaa ya Mpanda Paul swankala amesema kipindi cha masika huambatana na magonjwa ya mlipuko hivyo jamii inapaswa kuzingatia usafi ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa ya watu ambao wana tabia ya kutiririsha kinyesi wakati mvua inanyesha.