Mpanda FM

Jeshi la polisi Katavi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma ya mauaji

10 October 2023, 8:33 am

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kasta Ngonyani. Picha na Maktaba

Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo Dotto Mathias (37) kwa tuhuma ya mauaji

Na Ben Gadau – Katavi
Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo Dotto Mathias (37) kwa tuhuma ya mauaji yaliyotokea katika kitongoji cha kabatini kata ya mwese Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mpanda redio fm Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Kasta Ngonyani amesema tukio hilo limetokea October mwaka huu majira ya saa kumi jioni katika kitongoji hicho.

Sauti ya Kamanda Kasta Ngonyani

Aidha amewataja waliouawa kuwa ni Mariam Mtevu (13) na Esta Zubel Enock (2) huku akisema chanzo cha mauaji hayo ni baada ya mama wa Watoto hao kukataa kuwa na mahusiano na mmoja wa watuhumiwa hao.

Sauti ya Kamanda Kasta Ngonyani

Ngonyani ameendelea kuiasa jamii kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za matukio ya aina hiyo ikiwa ni sambamba na kutokomeza matukio hayo.

Sauti ya Kamanda Kasta Ngonyani