Mpanda FM

Mpanda: Wananchi waomba mchakato TASAF upitiwe upya

10 June 2023, 3:35 pm

MPANDA

Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kupitia upya mchakato wa upatikanaji wa kaya maskini ili kuuwezesha mpango wa kunusuru kaya maskini unafika kwa walengwa kama ilivyokusudiwa.

Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi hao wameonyesha kutoridhishwa na namna ya upatikanaji wa kaya ambazo zinapaswa kunufaika katika mpango huo jambo ambalo limeleta ukakasi kwa jamii mkoani hapa.

Kwa upande wake afisa ufuatiliaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini [TASAF] Manispaa ya Mpana Castory Alfred akizungumza na Mpanda Radio fm amesema kuwa mchakato wa upatikanaji wa majina ya walengwa huanzia ngazi za mitaa na vijiji na hakuna namna ambayo inaweza kutumika kuingiza majina ya watu wasiokidhi vigezo.

Kumekuwepo kwa malalamiko katika baadhi ya maeneo mkoani Katavi yanayotokana na baadhi ya wananchi kutoingizwa katika mpango huo huku wakidai kukidhi vigezo.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#tasaf