Mpanda FM

Wananchi Dirifu waomba ufafanuzi kuhusu RK

7 June 2023, 10:22 am

MPANDA

Wananchi wa kijiji cha Dirifu wameuomba uongozi wa mkoa wa Katavi kutolea ufafanuzi juu ya uwepo wa mwekezaji (Raymond Kamtoni RK ) katika machimbo ya mlima wa kijiji hicho.

Wakizungumza katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko uliofanyika katika kijiji hicho wananchi hao wameomba kufahamu juu ya mustakabali wa mwekezaji huyo katika kijiji hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kuwa mwekezaji RK yupo kisheria katika kijiji hicho huku akiendelea kuwataka wananchi kujiunga na kikundi cha Kagera Group ili waweze kuwa na nafasi ya kufanya maamuzi katika masuala mabalimbali.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#wizarayamadini