Mpanda FM

Mama afanya jaribio la kumuua mtoto baada ya kujifungua Katavi

19 January 2024, 12:54 pm

Mama wa Mtoto huyo akiwa katika hospitali hiyo kwa Matibabu zaidi ya Mtoto .Picha na Gladness Richard

Amefanya kitendo hicho baada   ya kufika hospitali  na kuomba kwenda chooni na huko ndipo alipofanya jaribio hilo.

Na Gladness Richard-Katavi

Binti anayefahamika kwa jina la Rehema Erick Mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Kijiji cha Mtapenda Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi anatuhumiwa kwa kujaribu kumuua Mtoto wake  Mara baada ya kujifungua katika Vyoo vya hospitali ya halmashauri hiyo.

Akizungumza na Mpanda Radio Fm Mama Mzazi wa Rehema Ambaye anajulikana kwa jina la Winfrida Deus  amesema kuwa binti yake amefanya kitendo hicho baada   ya kufika hospitali  na kuomba Kwenda chooni na huko ndiko alipofanya jaribio hilo.

Sauti ya Mama Mzazi wa binti aliyefanya tukio hilo akieleza ilivyokuwa

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo Glory Solomon Amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi na wamefanikiwa kumuokoa Mtoto huyo huku akiwa amepata Majeraha ya kuvunjika Miguu yote Miwili.

Sauti ya Daktari akieleza walivyobaini tukio lililofanywa na Mwanamke huyo na jitihada za kuokoa uhai wa Mtoto huyo

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amefika Katika hospitali hiyo kujua maendeleo ya Mtoto huyo huku akitoa   onyo kwa Wanawake wote wanaojaribu kukatisha uhai wa Watoto wao huku akiliagiza Jeshi la Polisi  kumchukulia hatua kali za Kisheria Bi.Rehema kwa kosa la kujaribu kumuua Mtoto wake.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akikemea vitendo hivyo kwa Wanawake

Tukio hilo limetokea siku ya Tarehe 18 Januari 2024 Katika hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo Baada ya Rehema kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kupata Matibabu.