Mpanda FM
Mpanda FM
9 September 2025, 8:41 pm

Leonard Victor afisa elimu manispaa ya Mpanda.Picha na Sumaiya Emmanuel
“Nimejiandaa vizuri na nafurahi kuhitimu elimu yangu ya msingi”
Na Sumaiya Emmanuel
Jumla ya wanafunzi 5312 wanatarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Akizungumza na Mpanda radio FM afisa elimu manispaa ya Mpanda Leonard Victor Rutta amesema maandalizi ya awali kuelekea mtihani huo yamekamilika na kueleza manispaa imeshakamilisha mipango kuelekea ufanyikaji wa mitihani hiyo.
Kwa upande wao Wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi manispaa ya Mpanda wamesema maandalizi kuelekea mitihani yao yamekamilika na kuwaahidi wazazi na walimu kufanya vizuri katika mitihani hiyo.
Kwa upande wao, baadhi ya wazazi wamesema wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na walimu pamoja na kuwaandaa watoto kisaikolojia ili kuondoa hofu na kuongeza hali ya kujiamini. Wameeleza kuwa motisha na malezi ya karibu ni silaha kubwa ya kuwasaidia watoto kufanikisha mtihani.