Mpanda FM

Mwenyekiti Chadema mkoa wa Katavi atangaza maandamano

19 April 2024, 12:03 pm

 Mwenyekiti wa Chama cha Chadema mkoa wa Katavi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Picha na Lilian Vicent

“tuna mambo makuu manne ikiwamo jambo la maandamano ambapo wiki ya maandamano inaanza tarehe 22 mwezi wa nne na jambo hili la maandamano lina umuhimu mkubwa,serikali inatakiwa irekebishe mambo mbalimbali”

Na Lilian Vicent-Katavi

Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema  wanatarajia Kuanza wiki ya  maandamano  kuanzia april 22 mwaka  2024  

Mwenyekiti  wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa katavi  Rhoda Kunchela ameyasema hayo  wakati akizungumza kwenye  mkutano na waandishi wa habari ,viongozi pamoja na wajumbe wa chama hicho    uliofanyika katika ofisi za Chadema mkoani hapa  na kuongeza kuwa  unyonywaji unaofanywa kwa wachimbaji wadogo ni sababu inayochangia maandamano.

Sauti ya Mwenyekiti  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa katavi  Rhoda Kunchela

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali wamesema wanaunga mkono na  watahamasisha  wananchi kujitokeza  kuandamana .

Sauti ya viongozi wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali

Nao wanachama walihodhuria kikao hicho wamesema kuwa  wao  wamepokea kauli ya viongozi wao na wanahitaji tume huru itakayosimamia uchaguzi kwa haki.

Sauti ya wanachama waliohudhuria kikao hicho

video ya habari hii inapatikana katika youtube channel yetu bofya hapa kutazama.