Mpanda FM

Wananchi Kapalala walia na maji safi, salama

28 July 2023, 4:15 pm

KATAVI

Baadhi ya wananchi wa vitongoji vya kata ya Kapalala halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameiomba serikali kuwaongezea mtandao wa upatikanaji wa maji safi na salama katika kata yao.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM wamesema baadhi ya maeneo ya kata hiyo bado hayajafikiwa na maji ya kutosha na kuziomba mamlaka husika kupitia mbunge wao kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mtakuja kata ya Kapalala, mbunge wa jimbo la Nsimbo mkoani Katavi Anna Lupembe amewahahikishia Wananchi wa kata ya Kapalala kupata maji safi na salama katika maeneo yote.

Aidha amesema kuwa kipindi mchakato wa upatikanaji wa maji kutoka vyanzo vya Ikolongo utakapokamilika wananchi wa kata ya Kapalala na vijiji vingine 28 vya halmashauri ya Nsimbo watanufaika na mradi huo.

#mpandaradiofm97.0

#ccmtanzania