Mpanda FM

Upatikanaji nishati ya mafuta Mpanda bado kizungumkuti

24 July 2023, 10:14 am

MPANDA

Kufatia kuwepo kwa mwendelezo wa changamoto ya uhaba wa nishati ya mafuta wananchi halmashauri ya manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kutatua changamoto hiyo.

Wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti wamesema kuwa serikali inapaswa kutafuta njia ya kutatua changamoto hiyo kwani inakwamisha shughuli.

Mpanda Redio FM kupitia kipindi cha Kumekucha Tanzania imezungumza na meneja wa mawasiliano na mahusiano kutoka Ewura makao makuu na amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo serikali ikiwa inaendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo

Ni takribani wiki mbili kumekuwepo na changamoto ya uhaba wa nishati ya mafuta hali ambayo inapelekea kuwepo kwa msongamano vyombo vya moto vikihitaji kupata nishati.

#mpandaradiofm97.0

#ewura