Mpanda FM
Mpanda FM
23 June 2026, 10:20 am

“Niwapongeze sana kufanya bonanza hili katika mkoa wetu wa Katavi”
Na Betord Chove
Watumishi wa taasisi zinazohusiana na kutoa haki wametakiwa kushirikiana ili kuweza kutenda haki kwa wananchi katika kutekeleza majukumu yao.
Wito huo umetolewa na Katibu tawala wa mkoa wa Katavi Albert Msovela akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hozza Mrindoko wakati wa bonanza lilioandaliwa na ofisi ya taifa ya mashitaka lilifanyika likihusisha wafanyakazi wa ofisi za mashitaka kutoka mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora.
Kwa upande wake Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Katavi Jaji geodfrey Ntemi Isaya akizungumza katika bonanza hilo ameshukuru ofisi ya mashitaka taifa kwa mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora kuchagua kufanya bonanza mkoani Katavi ambapo amewataka kuendeleza ushirikiano baina ya ofiisi ya mashitaka na mahakama ili waendelee kutenda haki kwa wananchi.
Wakizungumzia kuhusu dhima ya bonanza hilo wakuu wa mashikata kutoka mkoa wa Tabora na Kigoma wamesema kuwa ni kuleta umoja baina ya taasisi zote wanazofanya nazo kazi na kuwafanya wananchi waweze kuitambua ofisi ya taifa ya mashitaka na kazi wanazozifanya.
Bonanza hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia kwenye magunia, kukuna naz, kuvuta kamba, pamoja na mpira wa miguu ulohusisha timu ya Polisi Katavi na timu ya ofisi ya mashitaka kutoka mikoa ya Katavi, Kigoma na Tab