Mpanda FM

Wananchi Katavi waaswa juu ya matumizi holela ya dawa za kuzuia mbu

20 December 2023, 4:15 pm

Wananchi Katavi wameeleza mbinu wanazozitumia katika kuzuia na kupambana na ugonjwa wa malaria.

Na Gladness Richard – Mpanda

Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza mbinu wanazozitumia katika kuzuia na kupambana na ugonjwa wa malaria katika msimu huu wa mvua.

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wamesema  wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuchoma dawa ili kuangamiza mazalia ya mbu kwenye familia zao.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake mfamasia kutoka katika chuo cha ushirika cha Afya kilichopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi  Elia Kandonga ameanisha madhara yanayoweza kuwapata watumiaji wa mbinu za kuangamiza mbu bila kufuata masharti yaliyoainishwa.

Sauti ya Elia Kandonga