Mpanda FM

42 wanaswa Katavi wakiwa na bangi, wizi, pombe haramu

9 February 2024, 2:56 pm

Watuhumiwa 12 wamekamatwa wakiwa na mali za wizi,11 wakiwa na pombe haramu ya moshi,7 wakiwa na nyara za serikali na 12 wakiwa na madawa ya kulevya. Picha na Gladness Richard

Na Gladness Richard-Katavi

Jeshi la polisi     Mkoani Katavi limeendelea kufanya misako ,doria na Operesheni mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata jumla ya  watuhumiwa 42 kwa makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha mwezi January 2024.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Kaster Ngonyani  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuwa watuhumiwa 12 wamekamatwa wakiwa na mali za wizi,11 wakiwa na pombe haramu ya moshi,7 wakiwa na nyara za serikali na 12 wakiwa na madawa ya kulevya.

Ngonyani ameongezea kwa  kuwa kwa kipindi cha mwaka 2023 wamefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 822 na kufikishwa mahakamani wakituhumiwa kwa makosa ya jinai na kati yao 9 walihukumiwa kifungo cha maisha Jela.

Baadi ya gobole na pembe za wanyama zilizokamatwa na jeshi la polisi.

Jeshi la polisi linawaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya kihalifu ili mkoa wa Katavi uendelee kuwa sehemu salama.