Mpanda FM

60% ya familia Mpanda zatajwa kutelekezwa na mmoja wa wazazi

2 December 2023, 1:59 pm

Picha na Mtandao

Wanaume Wameonekana kuwa na Kiwango Kikubwa cha Utelekezaji wa Familia ikilinganishwa na Wanawake.

Na Gladness Richard-Katavi

60% ya Familia Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi zimetajwa kutelekezwa na  Mmoja wa Wazazi huku hali hiyo ikisababisha Watoto kutopata haki zao stahiki ikiwemo kutolelewa na Wazazi wa pande zote mbili.

Kutokana na takwimu hizo Wanaume wameonekana kuwa na Kiwango Kikubwa cha utelekezaji Familia ikilinganishwa na Wanawake

Wakizungumza na Mpanda Radio Fm Wananchi Mkoani hapa wametoa Maoni yao na kusema chanzo cha utelekezaji wa Familia unachangiwa na kuwa na kipato kidogo, Ulevi na tabia zingine zisizofaa.

Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoni Katavi wakitoa Maoni

Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Anilume Longo akizungumza na Mpanda Radio Fm amethibitisha kuwepo kwa asilimia hizo ndani ya Manispaa ya Mpanda huku akiwashauri Wazazi kuhudumia Familia zao.

Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Anilume Longo akizungumza.

Anilume amewashauri wanaotelekezwa kutoa taarifa katika Dawati la jinsia,Ofisi za Ustawi wa jamii na kwa Watendaji waliopo karibu yao ili Mtoto apate haki yake.