Mpanda FM

Chongolo hajaridhishwa na kasi ya mkandarasi ujenzi barabara Kibaoni – Mpimbwe

9 October 2023, 3:27 pm

Katibu mkuu CCM Daniel Chongolo hajaridhishwa na kasi ya Mkandarasi anaetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibaoni hadi Halmashauri ya Mpimbwe.

Na John Benjamin – Mlele
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo hajaridhishwa na kasi ya Mkandarasi anaetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibaoni hadi Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoani Katavi ikiwa na Urefu wa Kilomita 50 ambao kwa Sasa umefikia asilimia 11.2.

Chongolo amemtaka Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kuwasiliana na Mkandarasi na Wasimamizi wa mradi ili kubaini Sababu ya Kusuasua kwa Ujenzi ambao kukamilika kwake kutaongeza Tija kwa Wananchi wa Kibaoni na Sitalike.

Sauti ya Daniel Chongolo

Awali Akizungumza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Iddy kimanta amesema amesema licha ya changamoto hiyo kubainika kuna kilomita 40 kutoka Kibaoni -Mlele mpaka Sitalike bado fedha kwa ajili ya ujenzi huo hazijapatikana.

Sauti ya Iddy Kimanta

Ujenzi wa Barabara ya Kibaoni – Makutano ya Mlele unaogharimu zaidi ya Bilioni 80 ikiwa ni Fedha zinazotolewa na Serikali kwa asilimia 100 ni Utekelezaji wa Miongoni mwa ahadi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mkoani Katavi ikiwa ni kiunganishi kati ya makao Makuu ya mkoa wa Katavi na Rukwa.